
Mbunge wa jimbo la Kalenga Mkoani Iringa Mhe. Godfrey Mgimwa ametoa madawati 520 kwa ajili ya kutatua kero ya uhaba wa madawati katika shule zilizopo katika jimbo lake ikiwa ni hatua moja wapo ya kutekeleza agizo la Mhe. rais Dk John Pombe Magufuli juu ya uhaba wa madawati.
Akiongea na East Africa Radio Mhe. Mgimwa amesema katika hatua hiyo wafanyakazi wa halmashauri watatakiwa kuchangia madawati matatu, mkurugenzi madawati 10 huku wananchi nao wakichangia shilingi 5,000 ili kuhakikisha kero ya madawati inatatuliwa.
Mhe. Mgimwa amesema, katika kuhakikisha maendeleo ya elimu yanapatikana na kupata aendeleo endelevu ni vyema wadau mbalimbali wakajitolea kuisaidia serikali kuhakikisha inatatua kero za muda mrefu katika sekta ya elimu ikiwemo zikiwemo za madawati.
Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Dk. John Pombe Magufuli aliagiza wakuu wa mikoa yote nchini kuhakikisha ifikapo mwezi Juni mwaka huu katika maeneo yao wanashugulikia suala la uhaba wa madawati.