
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraim Kwesigabo, amesema hayo leo na kutaja sababu zilizochangia kupungua kwa kasi hiyo ya bei ya bidhaa na gharama kuwa ni kushuka kwa bidhaa takribani zote, za vyakula na zisizo za vyakula.
Kwa mujibu wa Bw. Kwesigabo, hali hiyo imeifanya thamani ya shilingi katika manunuzi kuimarika kiasi ambapo kila shilingi mia moja inaweza kufanya manunuzi yenye thamani ya shilingi 96 na kwamba kiwango cha sasa cha mfumuko wa bei hakina tofauti sana na ilivyo nchi nyingine za Afrika Mashariki isipokuwa Kenya tu ambako mfumuko umefikia asilimia 6.26.