Jumatano , 16th Jun , 2021

Mbunge wa Ilala na Mwenyekiti wa Bunge Mussa Azzan Zungu, ameitaka Wizara ya Viwanda na Biashara, kuhakikisha inafanya uchunguzi na ukaguzi kwenye Supermarket zote kubwa nchini kwa kile alichodai kuwa nyingi zimekuwa zikiuza sabuni feki za kuogea.

Mbunge wa Ilala na Mwenyekiti wa Bunge Mussa Azzan Zungu

Zungu ametoa kauli hiyo leo Juni 16, 2021, Bungeni Dodoma, wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Wizara ya Viwanda na Biashara.

"Wizara ya Viwanda na Biashara hebu tumeni watu wenu kwenye Supermarket kubwa, Dettol na sabuni za kuogea zote ni 'fake' watu wanalipa pesa nyingi wanatumia vitu siyo halali na pesa wanazolipa, chunguzeni Supermarket zote, kama Dettol ukiitia maji inakuwa nyeupe lakini leo ukiitia maji inakuwa nyeusi pamoja na sabuni ambazo zimeandikwa majina makubwa pia ni feki," amesema Mh. Zungu.