Jumanne , 25th Jun , 2019

Mbunge wa Ulanga Gudluck Mlinga, amehoji juu ya matumizi ya mipira ya kiume (Kondomu) kwa wanawake na wanaume, kwa kile alichokidai kuwa licha ya mipira hiyo kuwepo kumekuwa na idadi kubwa ya ongezeko la watoto wa mitaani.

Mbunge Mlinga ametoa kauli hiyo Bungeni Jijini Dodoma leo, wakati akiuliza swali la nyongeza kwenda kwa Wizara ya Afya Maendeleo Jamii Jinsia Wazee na Watoto, katika kikao cha 52 kilichoongozwa na Spika Ndugai.

"Licha ya watengenezaji wa mipira kuweka vionjo kwenye mipira ya kiume na kike lakini watoto wa mitaani bado wapo, Je Serikali ina mkakati gani kutoa elimu kuhusu matumizi ya mipira hii?".

Akijibu swali hilo, Mbunge Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile, amesema kuwa "rai yangu kwa jamii kabla hatujaingia kwenye suala la malezi, tujipange kwanza"

Kwa sasa Bunge linaendelea jijini Dodoma ambapo leo Bunge hilo linatarajiwa kupigia kura Mapendekezo ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020.