Jumanne , 21st Jun , 2022

Mbunge wa Singida Kaskazini Ramadhan Ighondo, ameishauri Wizara ya Fedha na Mipango, kuongeza kodi kwenye kucha na kope za bandia kama walivyoongeza kwenye mawigi.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Ramadhan Ighondo

Kauli hiyo ameitoa hii leo Juni 21, 2022, Bungeni jijini Dodoma, wakati wa akichangia hoja ya bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

"Kama ulivyoweka kodi kwenye mawigi, ongeza kodi kwenye kucha na kope ili haya ambo yasiletwe kutoka nje unaua viwanda vya ndani, hamasisha uzalishaji wa ndani, kwanza viwanda vitaleta ajira na kuongeza pato la ndani," amesema Mbunge Ighondo