Jumatatu , 10th Jul , 2023

Watu sita wakiwemo watoto watatu wameuawa katika shambulio la shule ya chekechea katika jimbo la kusini mashariki mwa China la Guangdong.

Polisi wanasema wamemkamata mwanamume mwenye umri wa miaka 25 kwa jina la Wu huko Lianjiang. 

Waathirika wengine ni mwalimu na wazazi wawili, shirika la habari la AFP liliripoti, likimnukuu afisa mmoja wa eneo hilo. Mtu mmoja pia alijeruhiwa.

Polisi wameiita kesi hii kuwa ni "shambulio la makusudi" lakini haijafafanuliwa juu ya sababu iliyopelekea tukio hilo.Shambulio hilo lilitokea Jumatatu  wakati wazazi walipokuwa wakiwaondoa watoto wao kwa ajili ya masomo ya majira ya joto.  

Lianjiang ina wakazi wapatao milioni 1.87.Wakati video za shambulio hilo zikisambaa katika mitandao ya kijamii ya China, zilizua hasira na mshtuko.

  Silaha za moto zimepigwa marufuku nchini China lakini nchi hiyo imeshuhudia mashambulizi ya kisu katika miaka ya hivi karibuni, ingawa pia kulikuwa na tukio moja ambapo mshambuliaji huyo alitumia dawa ya kemikali kuwajeruhi watoto 50.