Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mashambulizi ya risasi kuundiwa kikosi

Alhamisi , 14th Sep , 2017

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa imesema imepanga kuunda kikosi maalum kitakachohusisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama ili kupambana na matukio ya kihalifu ikiwemo mashambulio yanayohusisha silaha za moto

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi leo bungeni wakati alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Mkoani (CUF) Twahir Mohamed alipouliza ni kwa nini Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) lisihusishwe katika kukomesha matumizi ya silaha na mauji ya raia wasiokuwa na hatia yeyote nchini huku akitolea mfano kwa tukio la shambulio la Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mirataba pamoja na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambao wote walishambuliwa na risasi katika siku tofauti ndani ya mwezi huu.
 
Waziri Mwinyi amesema hapana shaka kuwa kazi ya Jeshi la ulinzi ni kulinda mipaka ya nchi, lakini pale linapohitajika kutoa msaada katika maeneo mengine, chombo hicho kipo tayari kufanya hivyo.

"Ni dhahiri kwamba kazi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania( JWTZ) ni kulinda mipaka, lakini pale ambapo linahitajika au linaombwa kusaidia mamlaka nyingine, iwe za kiraia au iwe vyombo vingine vya ulinzi na usalama, basi wanakuwa tayari kufanya hivyo", amesema Dkt. Mwinyi.

Pamoja na hayo, Waziri Mwinyi ameendelea kwa kusema "Kwa hali ilivyo sasa itaundwa 'task force' (kikosi maalumu) itakayojumuisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama, ili kuweza kulifanyia kazi tatizo hili la uvunjifu wa amani ndani ya nchi na sina shaka juu ya kazi hiyo kwa kuwa naamini imeshaanza", amesisitiza Waziri Mwinyi.

Kwa upande mwingine, Dkt. Mwinyi amewahakikishia Watanzania na kusema jukumu hilo litatekelezwa mapema ili hali ya usalama ipatikane ndani ya nchi.

HABARI ZAIDI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu

Mwili wa Boaz Sanga, Mwanafunzi wa CHuo cha SAUTI Mwanza baada ya kupatikana Pembezoni wa Ziwa Viktoria

Mwanafunzi wa SAUTI afariki akijaribu kuogelea

Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri, CDF Mpya wa Kenya

Luteni Charles Muriu ateuliwa kuwa CDF mpya Kenya

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa 124%

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita