Jumatano , 16th Dec , 2015

Mapigano yameibuka tena katika kijiji cha Tindigai ‘B’ wilaya ya Kilosa, Morogoro ambapo wakulima 11 wakiwemo mwenyekiti wa kijiji hicho na mwenyekiti wa kitongoji wamevamiwa na kupigwa na wafugaji na kupelekea kulazwa katika hospitali ya Kilosa.

Mganga mfawidhi hospitali ya wilaya ya Kilosa Dkt. Dickson Masele.

Majeruhi hao ambao ni wakulima wamesema kuwa ilikuwa majira ya asubuhi wakielekea mashambani ghafla walivamiwa na kundi la wafugaji wakiwa na slaha za jadi na kuanza kuwapiga bila sababu.

Kwa upande wao viongozi wa kijiji na kitongoji cha Tindiga ‘B’ ambao nao pia wamelazwa katika hospitali kufuatia kipigo hicho wameeleza walivyovamiwa na kundi la wafugaji na kupelekea mapigano hayo.

Mganga mfawidhi hospitali ya wilaya ya Kilosa Dkt. Dickson Masele amethibitisha kupokea majeruhi 11 wakiwemo wanaume tisa na wanawake wawili waliotoka kijiji cha Tindiga B wakiwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao na kwamba hali zao zinaendelea vizuri.