Maombi ya shukrani kuondoka kimbunga Jobo

Jumamosi , 1st Mei , 2021

Prophetess Trizah ambaye ni mtumishi wa kanisa la Rhema The Faithful Church, akiwa na waumini wa kanisa hilo leo wamefanya maombi katika fukwe ya Coco ya kumshukuru Mungu kwa kuiepusha nchi na kimbunga Jobo.

Waumini wakiwa kwenye maombi

Mtumishi Prophetess Trizah na waumini hao wamefanya maombi hayo leo Mei 1, 2021 ambapo ameeleza kuwa kuna kila sababu ya watanzania kumshukuru Mungu kwa kuwaepusha na janga hilo ambalo lingeleta madhara makubwa.

Zaidi tazama video hapo chini