Jumatano , 30th Aug , 2023

Watoto wawili wenye umri wa kati ya miaka mitatu wote wa familia moja katika mtaa wa Tulieni Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi, wamefariki dunia kwa kuungua na moto baada ya chumba walichokuwa wameachwa na wazazi wao kutekea kwa moto.

Mama wa watoto waliofariki kwa moto

Akizungumza Mama wa watoto hao amesema haelewi ni kipi kilitokea kwani aliwaacha watoto wake ndani kisha na yeye kwenda sokoni na kwamba hakuwa amewasha kitu chochote na mtungi wa gesi haukuwa na gesi kwani iliisha siku nyingi

Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto Wilaya ya Mpanda George Mwambungu amefika eneo la tukio na amethibitisha kutokea kwa vifo vya watoto hao.

Jeshi la Zimamoto wilayani Mpanda, limetoa rai kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya kuondoka nyumbani bila uangalizi wowote kwa watoto wao.