
Spika mstaafu, Pius Msekwa
Akizungumza leo Julai 15 na EATV/Radio Digital, Msekwa amesema kwamba yeye hana la kusema na kwamba kama analo atawatafuta wahusika, na si kila mtu anapaswa kujua.
''Ni barua nyingi zimekuwa zikielekezwa kwangu, lakini mimi sina neno kama nikiwa nalo ntawafafuta mwenyewe na sio lazima ninyi mjue'' amesema Pius Msekwa.
Kwa mujibu wa barua hiyo, Yusuph Makamba na Abdulrahman Kinana, wameamua kutokwenda mahakamani, kwasababu jambo hilo lina taswira ya kimkakati na lina mtandao wenye malengo ya kisiasa, hivyo linapaswa kushughulikiwa kisiasa. Lakini pia hawawezi kwenda mahakamani kudai fidia, kwa kuwa heshima yao haiwezi kufananishwa na fidia.
Isome hapa chini barua yao ya wazi.