Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Ametoa wito huo leo Julai 19, 2022, wakati akifungua maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kuzitaka taasisi zote za elimu ya juu kuendelea kufanya mapitio ya mitaala iliyopo kwa kuzingatia miongozo iliyopo ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira.
"Pamoja na kusimamia taaluma, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, pia iongeze jitihada katika kusimamia masuala ya utafiti na ushauri katika vyuo vikuu ili kuvifanya viwe chachu ya maendeleo na suluhisho la changamoto mbalimbali za maendeleo ya jamii yetu na Taifa kwa ujumla," amesema Waziri Mkuu
"Taasisi za Elimu ya Juu na zile za Utafiti na Maendeleo zishirikiane kwa karibu na sekta binafsi, hususan viwanda na kuweka utaratibu wa kuendeleza teknolojia zinazozalishwa nchini na kuhamasisha matumizi yake ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi," ameongeza Waziri Mkuu