Ijumaa , 20th Dec , 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amezitaja Sekta zinazoogoza kwa kuwa na migogoro ya kikazi, na kupelekea kutumika vibaya kwa rasilimali muda kati ya Mwajiri na Mfanyakazi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.

Waziri Mhagama ameyasema hayo Mjini Morogoro, wakati akifungua kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa Majukumu ya Tume, kilichowakutanisha wasuluhishi na waamuzi wa migogoro ya kikazi na wasaidizi wa Tume hiyo.

"2019 Sekta ya ulinzi binafsi ndiyo inayoongoza kuwa na migogoro mingi, sekta nyingine inayoongoza kuwa na migogoro mingi ni sekta ya Ujenzi, tunatamani migogoro isitokee kwenye Sekta hiyo, isizalishwe kwa sababu miradi mingi inazalishwa kwenye hii sekta." amesema Waziri Mhagama.

Aidha Waziri Mhagama ameongeza kuwa, "Sekta nyingine ambayo iljitokeza ni Sekta ya Biashara, Sekta nyingine ni ya Hotel, kila mwaka huwa inaongoza kwenye mgogoro, na 2018 mpaka 2019 Sekta ya Viwanda yenyewe imejitokeza kwenye migogoro." ameongeza.