Alhamisi , 16th Mar , 2023

Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imezuia kufanyika kwa mkutano mkuu wa Chama cha Walimu (CWT) uliotarajiwa kufanyika kesho Jiji Tanga baada ya aliyekiwa Katibu Mkuu Deus Seif na Mhazini Mkuu Alawi Aboubakary, kupinga kutimuliwa kwenye chama wakati wakiwa na kesi Mahakama Kuu Dar es Salaam.

Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma

Wakili wa upande wa waleta maombi Nashon Nkungu, akizungumza nje ya mahakama amesema uamuzi huo wa Mahakama Kuu, unatoa nafasi kusikilizwa kwa kesi ya msingi ya waleta maombi kuitaka Mahakama Kuu kutoa tafsiri ya mkutano mkuu wa nusu muhula wa CWT kuwajadili waleta maombi wakati wakiwa na kesi mahakamani.