Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, na mgombea mwenza wake Samia Suluhu Hassan wakiwapungia mikono wana CCM na wananchi.
Akiongea katika mkutano wa hadhara mkoani humo uliohudhuriwa na Maelfu ya Wakazi wa Mkoa huo Mh. Magufuli amesema ataondoa kero za kodi na wananchi na badala yake ataboresha viwanda na kutoa fursa kwa wawekezaji wazawa ili kukuza soko la Ajira.
Dkt. Magufuli amesema kuwa kilio cha Watanzania ni kuwa na uchumi utakaowawezesha kujikwamua katika umasikini hivyo sekta ya viwanda itakua na uwezo wa kuajiri watanzania wengi zaidi na kupunguza lundo la kodi linalowakabili.
Wakati huo huo Mgombea Mwenza wa Chama cha Mapinduzi CCM akiwa wilayani Bahi amesema endapo wananchi watakipa ridhaa ya kuendelea kuongoza kitaboresha kilimo cha umwagiliaji wa skimu katika nyanda kame hususani umwagiliaji wa skimu ya Mpuga katika wilaya ya Bahi.
Bi. Samia Suluhu amesema kuwa hali hiyo itawaondolewa wakulima kilimo cha kutegemea mvua zisizotabilika na zinazowafanya washindwe kuinua uchumi wao kupitia kilimo.
Bi. Samia ameongeza kuwa serikali ya CCM ilishatengeneza miundo mbinu ya umwagiliaji lakini bado kuna haja ya kuongeza juhudi ili kuwasaidia wakulima wanaotoka katika nyanda kame waweze kulima kwa biashara na kujitosheleza kwa chakula.