Jumanne , 23rd Oct , 2018

Watu wawili wamefariki na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea eneo la Igagala tarafa ya Mikumi katika Barabara Morogoro Iringa, ikihusisha malori mawili.

Pichani magari yaliyogongana.

Ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa saba imehusisha malori mawili aina ya Scania yenye namba ya usajiri T 247 CMT/T. 807 CMN mali ya kampuni ya Lake Oil iliyogongana na Scania yenye namba za usajili   za kugongana T. 430 BLZ/T. 527 BLY .

Akiongea na www.eatv.tv, leo Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Mugabo Wekwe amethibitisha kupokea taarifa ya ajali hiyo, iliyohusisha malori hayo mawili na kusema kuwa miili pamoja na majeruhi wamehifadhiwa hospitali ya wilaya ya Mikumi.

Kamanda Mugabo amewataja waliofariki kuwa ni dereva na utingo wa gari yenye namba T 430 BLZ ambao majina yao bado hayajafahamika na majeruhi ni dereva wa kampuni ya Lake Oil, Ivan  Thadei ambaye hali yake bado ni mbaya.