Ijumaa , 6th Jun , 2014

Diwani wa kata ya Bunju manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Bw. Majisafi Sharif, amekanusha tuhuma zilizotolewa bungeni na mbunge wa Kawe Bi. Halima Mdee kuwa yeye na madiwani wenzake wamehongwa pesa shilingi milioni 300.

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka.

Kwa mujibu wa Mdee, pesa walizohongwa madiwani hao ni kwa ajili ya kushawishi wananchi kukubali kiwango cha fidia kilichotolewa na mwekezaji katika mgogoro wa ardhi katika eneo la Chasimba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, diwani huyo amekanusha tuhuma za wao kuhongwa kiasi hicho cha pesa na kufafanua kuwa suala la fidia kwa wakazi wa Chasimba limeridhiwa na wakazi wote isipokuwa kikundi cha watu wachache aliosema wanataka kuukuza mgogoro huo kwa manufaa yao binafsi.