Jumanne , 15th Oct , 2024

Madereva wanaotoa huduma za usafiri kupitia mtandao wameandamana wakishinikiza kupungua kwa makato wanayotozwa na watoa huduma mtandaoni (commission) kutoka asilimia 25 mpaka asilimia 10. Kwani asilimia 25 wanayotozwa haina faida kwao

Moja ya madereva akizungumza kwa niaba ya madereva wenzake walipofika kituo cha Polisi Osterbay

Maandamano hayo ambayo yametia timu ofisi za tax mtandao (bolt) makao makuu Morocco na baadae kuelekea makao makuu ya Polisi Osterbay yamewakutanisha madereva hao na mkurugenzi wa watoa huduma mtandao na mkurugenzi LATRA na wameahidi kushughulikia changamoto zao walizo ziwasilisha.

“Kwa wengi wetu vijana tuliopo hapa hii ndo ajira yetu na madereva tunataka makato afadhali yangekuwa angalau asilimia 10 au 15 lakini sasahivi tunakatwa asilimia 24 au 25 ukiangalia kwenye trip ya elf 10,000 unakawa 2500 chombo ni cha kwako na mteja asipofika salama wewe ndo unawajibishwa” amesema Muslim Kiondo dereva bajaji

Aidha madereva hao wamelalamikia kitendo cha wao kutosikilizwa pindi wanapowasilisha changamoto zao wanazokumbumbana nazo kwa wateja na wateja kupewa kipaombele hali ambayo kama madereva wamesema hawakubaliani nayo na wametaka kupewa kipaombele kama wanavyosikilizwa wateja.