Jumatatu , 25th Jul , 2016

Maandalizi ya Maonyesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki, yanaendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Mkoani Morogoro kwa Shughuli mbalimbali ikiwemo ukarabati wa Miundombinu ya uwanja huo.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. KEBWE STEVEN KEBWE

Katibu wa Chama cha Wakulima Mashariki Rajab Mbonde amesema kuwa Maonesho ya mwaka huu yatakuwa ni ya 24 yatakayozihusisha za mikoa iliyopo katika kanda ya Mashariki ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Morogoro.

Akiongea mbele ya Mgeni rasmi wa Kikao kilichowashirikisha wakuu wa mikoa yote kutoka kanda ya Mashariki Dkt. Kebwe Steven Kebwe, Katibu huyo wa Chama cha wakulima amesema maandilizi yameanza katika nyanja zote ingawa kunachangamoto mbalimbali ikiwemo za ukarabati wa mabanda.

Akifunga Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambae ndie atakua mwenyeji wa Maonyesho hayo Dkt. Kebwe Steven Kebwe ametoa maagizo kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira kuhakikisha Maji yanapatikana eneo hilo Muda wote.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. KEBWE STEVEN KEBWE