Jumanne , 8th Sep , 2015

Baraza la Mitihania la taifa la Tanzania NECTA limesema jumla ya watahiniwa 775,729 wameandikishwa kufanya mtihani wa darasa la saba unaotarajiwa kuanza hapo kesho katika shule za msingi 16,096 zilizopo nchini.

Katibu mtendaji wa NECTA, Dkt.Charles Msonde

Akitangaza kuanza kwa mitihani hiyo itakayofanyika kwa Siku mbili leo jijini Dar es salaam,Katibu mtendaji wa NECTA, Dkt.Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa hao 361,502 in wavulana ambayo in asilimia 46.6 na wasichana 414,227 ambayo ni asilimia 53.4.

Kwa upande mwingine, DKt. Msonde amezitaka kamati za mitihani za mikoa na wilaya kuhakikisha taratibu za mitihani zinazingatiwa ikiwa ni pamoja kuepukana na udanganyifu na shughuli za kampeni kutoingilia katika maeneo ya vituo ya mitihani.

Katika hatua nyingine amewaasa wanasiasa kuacha kuendesha shughuli za kampeni maeneo ya karibu na vituo vya mitihani ili kuepuka kupunguza umakini wa wanafunzi hao katika ufanyaji wa mitihani hiyo.