Alhamisi , 14th Jul , 2016

Majeshi ya Ulinzi wa Amani na Usalama yanayolinda nchi zinazokabiliwa na vita yakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kushambuliwa na vikundi vidogo vya waasi vinavyomiliki silaha kwa ajili ya kufanya mashambulizi.

Brigedia Jenerali Yohana Mabongo akisalimia na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginald Mengi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa mafunzo ya pamoja kwa walinzi wa amani yanayojumisha nchi tatu, Tanzania, Marekani na Uingereza, Brigedia Jenerali Yohana Mabongo, amesema changamoto hiyo mara nyingi inawalazimu walinzi hao wa amani kuingia vitani ili kujilinda.

Brigedia Jenerali Mabongo amesema mafunzo hayo yanayojumisha mataifa hayo makubwa ya lengo na kupambana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika mataifa ambayo nchi hizo zimepeleka wanajeshi wake kwa ajili ya kulinda usalama na amani kwa wakazi wa maeneo husika.

Aidha Mkurugenzi huyo wa Mafunzo hayo ameongeza kuwa kuna changamoto nyingine nyingi ambazo wanakumbana nazo wakati wakiwa maeneo yao ya kazi ikiwemo lugha,tamaduni, mazingira ambayo hawajazoea,

Ameongeza pia kuna makosa madogo madogo ambayo yanafanywa na baadhi ya wanajeshi yanakuzwa na vyombo vya habari na kuonekana walinzi hao wa amani wanakiuka haki za binamu kwa kiasi kikubwa wakati hiyo huwa inakua ni kasoro ndogo kuzidi yale mengi masafi wanayoyafanya katika kazi yao hiyo.

Sauti ya Brigedia Jenerali Yohana Mabongo