
Kocha wa timu ya soka ya Yanga Mwinyi Zahera
Akizungumza kwenye kipindi cha East Afrika Breakfast cha EA Radio, Zahera amedai nchi za Ulaya zimekuwa mfano bora pindi mmoja anaposhinda uchaguzi husika mpinzani wake amekuwa akimpigia simu na kumpongeza kwa ushindi japo kwa upande wa Afrika hali ni tofauti ambapo vyama vingi vya upinzani vimekuwa vikilalamikia matokeo.
"Unajua Congo kila mara uchaguzi unapofanyika huwa kuna vurugu lakini sio Congo tu ni Afrika nzima anayeshindwa huwa hakubali matokeo, lakini niwaombee kwa Mungu awapitishe kwenye kipindi hiki kigumu ili kusiwe na fujo." amesema Zahera.
Raia wa Congo walipiga kura Desemba 30 mwaka jana ambapo matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa Januari 6, 2019 na matokeo rasmi yakitangazwa Januari 15, 2019 huku kura za awali zikimuonesha mgombea Emmanuel Ramazani Shadary, anayeungwa mkono na Rais anayeondoka Joseph Kabila akiongoza kwa idadi ya kura.