Jumanne , 30th Jun , 2015

Takwimu zinaonesha kuwa nchini Tanzania takribani watu tisa kati 100 wana ugonjwa wa kisukari na kwenye kila watu wazima watatu mmoja ana tatizo la shinikizo la damu huku magonjwa hayo yasiyoambukiza yakizidi kuongezeka.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bw. Hauson Rweumbiza amesema inakadiriwa kuwa kisukari pekee kimeathiri maisha ya watu takribani milioni 371 duniani huku asilimia 80 wakiishi nchi zenye uchumi wa kati na masikini.

Rweumbiza amesema kuwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na zilizoendelea pia hazina rasimali za kutosha kuribu watu wote wanaobainika na ugonjwa wa kisukari na magonjwa mengine yasiyoambukiza.

Amesema kuwa gharama ya kukabiliana na mgonjwa yasiyo ya kuambukiza duniani kote ni mabilioni ya dola na hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa rasilimali finyu zilizopo.