Naibu Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Dkt. Khamis Kigwangala
Akiongea na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala amesema licha ya jitihada za serikali kutokomeza ugonjwa huo lakini bado kuna baadhi ya wataalamu wa afya pamoja na wanajamii wanaendelea kuwa chanzo cha kuenea kwa ugonjwa huo.
Mhe. Kigwangala amesema kumekuwepo na tabia ya wataalam hao wa afya pamoja na wanajamii kuficha wagonjwa pamoja na kutoa taarifa ya wagonjwa wachache kuliko uhalisia kunakwamisha juhudi za serikali kutokomeza ugonjwa huo.
Naibu waziri huyo ametumia fursa hiyo kuzitaka mamlaka husika kutoa taarifa sahihi za wagonjwa ili kurahisisha njia za kupambana na ugonjwa huo ambao umeripotia karibu mikoa yote nchini Tanzania.
Aidha amewataka viongozi wa mikoa na wilaya kutokutoa kauli za kuwatisha wataalamu wa afya na viongozi wa ngazi za chini kwa kigezo cha wagonjwa wa kipindupindu kwani kwa kufanya hivyo wataongeza kasi ya jamii kuwaficha wagonjwa wa kipindipindu.