
Hapi ametoa kauli hiyo mkoani Iringa wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusiana na waraka uliotolewa hivi karibuni na Makatibu Wakuu Wastaafu wa CCM, Abdurlhaman Kinana na Yusuph Makamba.
Hapi amesema kuwa "mimi nasema wazee wetu wamekengeuka, hata kama walikuwa na maoni wao ni wastaafu walikuwa na nafasi ya nzuri ya kuwasilisha maoni yao, tunashawishika kuamini ziko njama za kumdhoofisha Rais wetu kwa jitihada za kujenga nchi yetu."
Kuhusiana na Membe Hapi amesema kuwa "Membe alianza tangu tarehe 22,na 23 Januari 2016, akiwa mjumbe wa NEC alizungumza na vyombo vya habari, alikosoa na kubeza na wakati huo Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwa ni Nape Nnauye, na Katibu Mkuu akiwa Kinana"
"Membe alishindwa akiwa Waziri ataweza leo akiwa mwananchi wa kawaida? Najua kuna watu watasema kwanini Mkuu wa Mkoa unasema, ukimshambulia Rais unamshambulia mkuu wa mkoa mimi ni mwakilishi wa Rais, tutamlinda Rais wetu" ameongeza Hapi
Hivi karibuni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, kulianza kusambaa kwa sauti zinazodaiwa kuwa ni maongezi kati ya Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Kinana pamoja na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.