Jumanne , 27th Sep , 2022

Kimbunga Ian kimepiga Magharibi mwa Cuba kikiwa na upepo mkali unaofikia kilometa 205 kwa saa.

Mamlaka za Cuba zimetangaza hali ya dharura kwenye maeneo sita nchini humo, huku mamlaka za hali ya hewa zikionya uwepo wa mafuriko na maporomoko ya udongo. 

Maelfu ya watu wameaambiwa waondoke kwenye makazi yao na kutafuta makazi mengine. Kimbunga Ian kinategemewa kujiimarisha kuelekea jimbo la Florida, ambapo kwa mujibu wa gavana w ajimbo hilo kukatokea janga.  

Vimbunga zaidi vinatarajiwa kwenye ukanda wa pwani ya Florida siku ya kesho ambapo majanga hayo yanatarajiwa kuanza usiku wa jumanne hii.