Jumatano , 3rd Jul , 2024

Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara linamshikilia Mohamed Omary mzee mwenye umri wa miaka 70 mkazi wa kijiji cha Kiru mkoani Manyara kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye ulemavu wa miguu wa miaka 11 wakati akiwa nje ya nyumba yao.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Manyara George Katabazi

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Manyara George Katabazi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo majira ya jana asubuhi Julai 2, 2024, na kusema kuwa timu ya uchunguzi ipo katika eneo hilo kufanya uchunguzi ili kubaini sababu ya ukatili huo uliofanyika kwa mtoto huyo.

Wananchi nao hawakuwa mbali kutoa hisia zao kuhusu tukio la ubakaji  lililofanyika kwa mtoto huyo.