Jumanne , 16th Nov , 2021

Mkazi wa Kijiji cha Mavanga kilichopo Kata ya Mavanga wilayani Ludewa mkoani Njombe, anayefahamika kwa jina la Afro Nyigu (31) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumbaka mnyama aina ya nguruwe.

Nguruwe

Akizungumza Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Ramadhani Kihanga, amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 14, 2021, ambapo mtuhumiwa huyo alifika katika machinjio ya wanyama hao huku akiwa amelewa na kukuta nguruwe akiwa amefungwa kamba kwa maandalizi ya kuchinjwa ndipo kijana huyo alimvamia na kushiriki naye mapenzi.

Amesema wakati akiendelea na tendo hilo mlinzi wa machinjio hiyo alikuwa ametoka kidogo na aliporejea alimkuta kijana huyo akiendelea kufanya kitendo hicho ambapo alimkamata na kumpigia simu balozi na mtendaji wa kijiji ambao walifika katika eneo hilo la tukio.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa mara baada ya kumhoji mbakaji huyo wa nguruwe sababu za kufanya kitendo hicho alidai ni maamuzi yake binafsi hivyo hapaswi kuulizwa na ndipo walipomkamata na kumkabidhi mikononi mwa polisi.