Kenya yasitisha safari za Uingereza

Jumanne , 6th Apr , 2021

Shirika la Ndege la Kenya Airways limesitisha safari zake kuelekea Uingereza kufuatia mzozo wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili, hivyo watu wanaotaka kusafiri kwenye mataifa hayo wametakiwa kufikia tarehe tisa mwezi huu, kabla ya hatua hiyo kuanza kutekelezwa.

Wizara ya mambo ya nje ya wingereza ilikuwa ya kwanza kutoa ilani kwa raia wanaosafiri wingereza kutoka Kenya na mataifa mengine Afrika, ilani iliyotolewa na kuwataka wasafiri na ndege zote zinazotoka mataifa hayo kusitisha safari zake, ikitaja maambukizi ya virusi vya corona kuwa chanzo cha hatua hiyo.

Kenya kwa upande wake ikijibu Uingereza, ilisema kuwa hatua hiyo imaonyesha mapendeleo na ubaguzi, kwani taifa hili linaendelea kuchukuwa tahadhari zote kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni, hivyo haikustahili kuwa kwenye orodha ya mataifa yanayozuiliwa kuenda wingereza.

kwa taarifa ya Wizara ya mambo ya Nje ya Kenya kwa vyombo vya habari, imeijibu uingereza kwa kuwawekea vikwazo raia wa uingereza wanaosafiri kuingia Kenya, au ndege zozote zinazo tokea huko Uingereza ambapo ni sharti raia wake wawekwe karantini ya lazima kwa siku kumi nane, kinyume na ilivyokuwa awali na watahitajika kulipia karantini hiyo pamoja na kuhitajika kupimwa corona mara mbili.

Kenya inaeleza kuwa hatua ya Uingereza kwa mataifa hayo ya afrika yaliyotajwa kwenye orodha hiyo inaonyesha ubaguzi na maendeleo, ikisema kuwa hii itavuruga uhusiani mwema kati ya mataifa hayo na uingereza kibiashara, utalii na sekta zingine muhimu.