Alhamisi , 27th Mei , 2021

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, amewataka Watanzania kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama punde tu wanapoona viashiria vya ujambazi ili viweze kufanya kazi iliyokusudiwa na kutokomeza vitendo hivyo na kwamba serikali inahakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuwepo.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 27, 2021, Bungeni Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Makete Festo Sanga, lililohoji ni nini kauli ya serikali kufuatia vitendo vya ujambazi vilivyochipukia siku za hivi karibuni katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Dodoma.

Tazama video hapa chini