Jumatano , 28th Jul , 2021

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, leo Julai 28, 2021, amechoma chanjo Johnson & Johnson inayotolewa kwa dozi moja tu, ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona ambapo amesema kuwa amefanya hivyo kwa hiari yake mwenyewe baada ya wanasayansi kujiridhisha na usalama wa chanjo hiyo.

Rais Samia Suluhu Hassan wakati akijiandaa kuchoma chano ya Corona

Kauli hiyo ameisema leo Ikulu ya Dar es Salaam, ambapo amesisitiza kwamba yeye ni Mama, Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, Bibi na mke pia, hivyo asingejipeleka mwenyewe kwenye kifo licha ya kuwa na majukumu mengi kwenye Taifa.

Tazama video hapa chini