Alhamisi , 5th Mar , 2020

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi mkoani Singida, kumnyima dhamana Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema na kuendelea kumshikilia bila hata kumpeleka mahakamani.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema

Kufuatia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chama hicho, Tumaini Makene, imedai kuwa chama kimeamua kuchukua hatua za kisheria ili kuhakikisha Lema anapata haki zake, ikiwemo kuachiwa huru kwa dhamana au kufikishwa mahakamani.

Mbunge Lema anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida kwa mahojiano, tangu Machi 2, 2020, baada ya kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu vifo vya watu 14 wilayani Manyoni.