Jumatatu , 2nd Oct , 2023

​​​​​​​Wizara ya afya ya Misri imesema watu 38 wamejeruhiwa katika moto mkubwa uliotokea katika jengo la polisi mjini Ismailia.Watu 24 wametibiwa hospitalini kwa kuvuta moshi pamoja na wawili kwa ajili ya kuungua.

Waziri wa mambo ya ndani ameagiza uchunguzi ufanyike kuhusu moto huo, pamoja na "ukaguzi wa usalama wa miundombinu" wa kituo hicho.

Hakukuwa na taarifa za majeruhi au kama kuna watu waliokamatwa wakati moto huo ulipoanza.

Magari 50 ya kubebea wagonjwa yalipelekwa katika makao makuu ya Kurugenzi ya Usalama pamoja na ndege mbili za kijeshi. Watu 12 waliojeruhiwa hawakupelekwa hospitali na walitibiwa katika eneo la tukio.

Kuna hofu kwamba idadi ya watu waliojeruhiwa inaweza kuwa kubwa zaidi, huku mwandishi mmoja wa habari wa Misri akiripoti kwamba kutokana na ukubwa wa moto huo, kunaweza kuwa na vifo.

Mashahidi wawili waliozungumza na shirika la habari la Reuters walisema kuwa wazima moto awali walipambana kudhibiti moto huo, lakini vyombo vya habari vya eneo hilo vinasema kuwa baada ya zaidi ya saa tatu walifanikiwa kuudhibiti.