Ijumaa , 14th Jun , 2024

Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Lindi imemhukumu Mohamed Said Selemani mwenye umri wa miaka 62 mkazi wa kijiji cha Ng'apa wilaya ya Lindi, kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne.

Mtuhumiwa alitenda kosa hili Aprili 22, 2024 katika kijiji cha Ng'apa wilaya ya Lindi na kumsababishia maumivu makali mtoto huyo.

Hukumu hiyo ya kesi namba 11774 ya mwaka 2024 imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Maria Batulaine huku upande wa Jamhuri uliokuwa ukiongozwa na John Remi ambapo ulileta mashahidi watano pamoja na vielelezo karatasi ya polisi fomu namba 3 (PF 3) pamoja na cheti cha kuzaliwa.