Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, leo amemteua Jaji kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Jacob Mwambegele kufanya uchunguzi wa mgogoro wa mipaka ya Kijiji cha Mwabegere na vijiji jirani Mkoani Morogoro.
Mh. Lukuvi ametangaza uteuzi huo baada ya hatua mbalimbali zilizofanywa na ofisi yake kushindwa kupata ufumbuzi wa migogoro katika vijiji hivyo hali ambayo kama ingeachwa ingesababisha hasara kubwa kwa taifa hasara kwa upande wa fedha kwa kuwa zingetolewa pesa nyingi ambazo zisingeweza kuzaa matunda ya kupata suluhishi hilo.
Kwa upande wake, mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven Kebwe amewataka wakazi wa mkoa wa Morogoro na wawekezaji kutoa ushirikiano katika kutatua tatizo hilo ili shughuli za uzalishaji zifanyike kwa usalama na kuliongezea taifa kipato hivyo kuwa nchi ya uchumi wa kati


