
Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu Jaji Sylvain Ore (Wa kwanza kulia), akiwa na ujumbe wake walipotembelea IPP Media mkoa wa Dar es Salaam
Jaji Ore ametoa kauli hiyo hii leo Mei 21, 2021, alipotembelea ofisini hapa na kujionea jinsi ambavyo vinaendesha shughuli zake, ikiwemo suala la uchapishaji na uzalishaji wa magazeti kutoka The Guardian, masuala ya burudani, michezo na habari kutoka East Africa TV na East Africa Radio, ITV na Radio One, Capital TV na Capital Radio.
Aidha kwa upande mwingine Jaji Ore amekiri kwamba ziara yake hiyo ameifurahia kwani amepata uzoefu mpya katika masuala ya habari, kwani vyombo hivyo vimekuwa kama taswira ya vyombo vingine vya habari.