Jumamosi , 29th Mei , 2021

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewataka askari kuhakikisha wanaendelea kutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia na kushirikiana nao katika kuzuia na kupambana na uhalifu nchini.

IGP Simon Sirro

IGP Sirro amesema hayo Dar es Salaam, wakati akizungumza na baadhi ya wananchi wa eneo la Kawe wilayani Kinondoni ambapo amewataka wananchi kuacha kutoa rushwa kwani kitendo hicho ni kinyume na sheria za nchi.

Aidha, IGP Sirro ameendelea kuwasisitiza viongozi wa serikali hasa Watendaji wa Kata na Wenyeviti wa serikali za Mitaa kuwashirikisha wananchi katika vikundi vya ulinzi shirikishi ili maeneo yao yaendelee kuwa salama.