
- kufanya kazi za kilimo kama vibarua.
Mpango huo umetangazwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala mwishoni mwa ziara yake iliyomfikisha katika wilaya zote na katika maeneo ya mpaka na nchi jirani mkoani Kigoma ambapo amesema vibali hivyo vya miezi mitatu vitawezesha raia hao kutambuliwa na serikali kupata fedha na kutambua wako wapi na idadi yao.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema uamuzi huo wa idara ya uhamiaji utasadia kupunguza uhalifu na kuongeza tija katika kilimo pamoja na kujenga mahusiano mazuri na nchi jirani ya burundi ambayo raia wake wanaongoza kwa kuja nchini kufanya vibarua bila ya kibali na hivyo kuongeza idadi ya wahamiaji haramu.