Alhamisi , 28th Jul , 2016

Idara ya Uhakiki wa Mali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetakiwa kuacha kuzembea katika kusimamia manunuzi ili kuondoa ubadhirifu katika idara hiyo ambayo ni muhimu katika ukuaji wa uchumi.

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. , Khalid Salum Mohamed,

Akizungumza na watendaji wa mali za uhakiki visiwani Zanzibar, Mjini Unguja Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. , Khalid Salum Mohamed, amesema fedha nyingi za serikali zimekuwa zikitumika kwa ajili ya manunuzi hivyo ni vyema wakazingatia suala hilo.

Dkt. Mohammed amesema kuwa amtendaji yoyote ambae anaehusika na kuaulisha mali za serikali kinyume cha sheria kuachama mara moja ili kuweka matumizi bora ya fedha za serikali.

Idara hiyo ya Uhakiki wa mali ya serikali ya Mapinduzi Zanzibari inakadiriwa kuwa kwa kila mwaka kufanya matumizi ya serikali asilimia 70 ya fedha zinazoidhinishwa katika bajeti.

Sauti ya Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. , Khalid Salum Mohamed,