Mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo inayohudumia mikoa ya kanda ya ziwa Prof. Dk. Kien Mteta, amesema upasuaji huo umefanikiwa baada ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Kikwete kuipatia hospitali hiyo kifaa cha upasuaji katika idara ya upasuaji.
Mkuu wa kitengo cha upasuaji wa moyo na vichwa katika hospitali hiyo Dkt. William Mahalu anasema huduma ya upasuaji wa moyo inayofanywa na madaktari bingwa katika hospitali hiyo, huduma ambayo awali ilikuwa ikifanyika nchi za nje kwa gharama kubwa, sasa inafanyika katika hospitali hiyo kwa gharama nafuu na shabaha ni kufanya upasuaji kwa watu wanane kila mwezi.
Timu ya waandishi wa habari ikiongozwa na baadhi ya madaktari bingwa wa idara ya upasuaji ilifika hadi katika chumba cha upasuaji kujionea jinsi madaktari bingwa wanavyofanya upasuaji wa moyo kwa mgonjwa mmoja na kisha wametembelea wodi ya wagonjwa mahututi wanaohitaji uangalizi maalumu ICU na pia wakahimitisha kwa kuzuru kwenye wodi ya watoto waliofanyiwa upasuaji wa moyo.