Jumapili , 9th Jul , 2023

Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini imeteketeza hekari 310 za mirungi wilayani Same mkoani Kilimanjaro katika vijiji vya Rikweni, Heikondi na Mahande.

Mirungi ikiteketezwa

Kwa mujibu wa Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo, Aretas Lyimo, amesema operesheni hiyo ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais katika kukomesha kilimo cha dawa za kulevya nchi nzima.

Amesema Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama itaendelea kufanya oparesheni za mara kwa mara katika maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha kilimo cha mirungi na bangi kinatokomea kabisa nchini.