Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Akiongea katika Hotuba yake kwa wananchi kwa kila mwisho wa mwezi Rais Kikwete amesema kuwa matukio hayo ambayo yaliibuka mwaka 2006 Serikali iliweza kukabiliana nayo na mpaka kufikiwa mwaka 2011 kukawa hakuna tukio lolote la mauaji ya watu hao.
Aidha rais Kikwete ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuwafichua watu wote wanajihusisha na biashara ya viungo vya watu wenye Albinsim ili kwa pamoja kukomesha mauaji ya watu hao.
Kikwete amesema ni ujinga uliokithiri kwa mtu kutegemea ushirikina hasa kuwa na viungo vya ulemavu wa ngozi ndio kuna kufanya mafanikio katika shughuli zao hivyo kutaka juhudi zifanyike kueleimisha juu ya kuacha watu kuamini imani potofu.
Aidha Rais Kikwete amesema atakuata na watu wenye Ulemavu wa ngozi wiki ijayo ili kusikiliza maoni yao juu ya nini kifanyike katika kusaidiana kukomesha mauaji dhidi yao.
Katika hatua nyingine Rais Jakaya Kikwete amesema kazi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura nchini kwa kutumia mfumo wa BVR katika Halmshauri ya Makambako mkoani Njombe imevuka lengo la tume hivyo kulazimu kuongeza muda ili wananchi wote waliojitokeza waweze kujiandikisha.
Tume ilitegemea kuandikisha wapiga kura 9541 katika halamashauri hiyo lakini kutokana na mwitikio wa wananchi wameandikishwa watu 13.042.
Aidha Rais Kikwete amewataka viongozi wa vyama vya siasa,Serikali,dini na asasi za kiraia kuungana na tume katika kuwahamasisha wananchi kujiandikisha badala ya kuwachanganya kwa kutoa taarifa zisizo za kweli.