
Kamanda Lazaro Mambosasa amethibitisha taarifa hizo bila ya kutaja sababu zilizopelekea Mhe, Rungwe kukamatwa kwake
Rungwe ambaye alikuwa miongoni mwa wagombea urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, pia amekuwa miongoni mwa wanasiasa ambao wamekuwa wakiikosoa serikali mara kwa mara katika utendaji kazi wake, na hivi karibuni aliitaka serikali imalize mgogoro na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd iliyozuia ndege aina ya bombardier Q400- Dash 8 iliyonunuliwa nchini Canada.