Alhamisi , 2nd Jun , 2016

Wizara ya afya maendeleo ya jamii ,jinsia, wazee na watoto kupitia idara ya maendeleo ya jamii inazitaka halmashauri zote nchini kutoa kuipaumbele katika kuajiri maafisa maendeleo ya jamii kwani uhitaji wao ni mkubwa sana kwenye jamii.

Akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi msaidizi wa vyuo vya maendeleo ya jamii Neema Ndoboka amesema kuwa ni asilimia 44 pekee ya kata zote nchini ambazo zinamaafisa maendeleo ya jamii wakati maafisa wengi wamepata mafunzo na wapo mtaani hawana ajira yoyote.

Aidha Bi Ndoboka amesema kuwa uhaba wa maafisa ustawi wa jamii unaleta matatizo mengi kwenye jamii ikiwa ni pamoja na kupunguza nguvu ya mchango wa jamii katika kujua mahitaji yao.