Jumatatu , 26th Sep , 2022

Watu watatu wamepoteza maisha , wawili kati yao wakiwa ni watoto baada ya jengo la makazi lenye ghorofa tano kuanguka huko nchini Kenya, katika Kaunti ya Kiambu.

Tukio hilo limetokea Jumatatu ya leo  Septemba  26 2022.

Akithibiisha kutokea kwa tukio hilo mapema asubuhi ya leo, Kamanda wa polisi wa kaunti ya   Kiambu   Perminius Kioi , amesema kwamba shughuli za  utafutaji manusura zinaendelea . 

Ameongeza kuwa watu watatu wameokolewa kwenye tukio hilo na kukimbizwa hosptali kwa ajili ya matibabu.