
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala amesema kuwa wataalam kutoka wizara ya Kilimo, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, kama hawata toa ripoti maalum kuhusu funza hao kutakwamisha jitihada za serikali za kuelekea uchumi wa kati.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa watawasiliana na wataalamu hao ili wafanye uchunguzi zaidi wa kujua ni namna gani wanaweza kuzalisha zao hilo kwa ajili ya manufaa ya nchi kuliko kuacha kiwanda hicho kife wakati kina miundombinu yote ya kuzalisha nguo na nyuzi.
Kwa upande wake Mwekezaji wa kiwanda hicho amesema kutokana na hali hiyo alituma maombi serikalini kwa ajili ya kubadilisha matumizi ya kiwanda hicho ili aweze kuendeleza kiwanda hicho ili kilete tija kwake na taifa kwa ujumla.