Jumatatu , 15th Mei , 2023

Waziri Mkuu Kassim Majaiwa, amewataka wafanyabishara wa Kariakoo kuendelea na biashara zao kama kawaida na kwamba kikao cha Jumatano watakachokutana kitajadili na kupitia changamoto zote zilizopelekea wao kuanzisha mgomo huo hii leo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wafanyabiashara Kariakoo

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 15, 2023, jijini Dar es Salaam, alipofika katika eneo la soko la Kariakoo kwa lengo la kuzungumza na kuwatuliza wafanyabiashara hao waliokuwa wamefunga maduka wakiilalamikia TRA pamoja na kamatakamata ya mizigo wanayokumbana nayio.

"Keshokutwa Jumatano, nimeitisha hicho kikao kikubwa cha kupitia changamoto zenu zote, kero matatizo na kero zenu zote, tukutane tupo tayari kuwasikiliza tunataka tuondoe changamoto za wafanyabiashara, nawaomba sana mkubali ombi la serikali, fungueni maduka hata sasa hivi wateja wapo, fungueni maduka matatizo yenu tutayajadili Jumatano Anatoglo" amesema Waziri Mkuu