Ijumaa , 10th Jun , 2022

Familia ya aliyewahi kuwa mbunge wa Mikumi Joseph Haule, maarufu kwa jina la Professor Jay, leo imetoa shukrani zake kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa maamuzi yake ya kusema kwamba matibabu ya ugonjwa wa Professor Jay yatasimamiwa na serikali.

Mke pamoja na Mdogo wa Professor Jay

Wakizungumza hii leo Juni 10, 2022, jijini Dar es Salaam, mke pamoja na mdogo wa Professor Jay, wamewashuru pia Watanzania kwa sala na michango yao ya hali na mali waliyokuwa wakiitoa kwa siku zote 127 alizokuwa akitibiwa Professor kwenye hospitali ya Taifa Muhimbi.

Tazama video hapa chini