Ijumaa , 29th Mar , 2024

Familia ya mtoto aliyefanyiwa ukatili imekanusha kuwa hawana ndugu yeyote anayeitwa Benjamin Augustino wala kwenye familia yao hakuna mtu aliyekamatwa kutokana na sakata hilo.

Bibi wa mtoto aliyelawitiwa

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa ambazo zimeanza kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mjomba wa mtoto huyo aliyetajwa kama Benjamin Augustine ambaye amekamatwa kwaajili ya mahojiano na uchunguzi kama amewahi kuhusika kumfanyia mtoto ukatili huo akiwa nyumbani. 

Akiongea na EATV asubuhi ya leo Machi 29, 2024 Bibi wa mtoto huyo amesema kwenye familia yao hakuna mtu mwenye jina la Benjamin upande wa baba wala wa mama na wao wanashangaa kuona kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna ndugu yao amekamatwa.

Aidha ameiambia EATV, mtu pekee wanayemfahamu mwenye jina la Benjamin ni mtoto ambaye alikuwa anaishi jirani na hapo ambae alikuja mwaka jana 2023 likizo ya kusubiri kuanza kidato cha kwanza baada ya kumaliza darasa la saba mkoani Mtwara.

Bibi anasema huyo Benjamin ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza mkoani Mtwara na kaka yake na Benjamin ni dereva wa bodaboda ambaye jana Machi 28, alikuwa akiwatembeza polisi kwa ajili ya kufanya uchunguzi kwa majirani kuhusu tukio hilo.