Jumatatu , 29th Jun , 2015

Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji EWURA imetoa onyo kali kwa wafanyabiashara watakaothubutu kuficha mafuta kwa kisingizio cha bei mpya au kukosekana kwa mafuta.

Mkurugenzi mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi

Akizungumza kwa njia ya simu katika kipindi cha HOT MiX kinachorushwa na EATV kuanzia saa 12 jioni, mkurugenzi mkuu wa EWURA Felix Ngamlagosi, amekanusha taarifa zilizosambaa kuwa mafuta yatakosekana katika siku mbili zijazo, na kusisitiza kuwa akiba ya mafuta iliyopo inatosha kutumika kwa zaidi ya wiki 2.

Ngamlagosi amesema mfanyabiashara yoyote atakayebainika kuficha mafuta atachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni na kifungo gerezani.

Msikilize hapa mkurugenzi mkuu wa EWURA akifafanua zaidi.........

Mkurugenzi mkuu wa EWURA akizungumzia taarifa za kukosekana kwa mafuta zilizoenea
Mkurugenzi mkuu wa EWURA akizungumzia athari za ongezeko la tozo katika bei ya mafuta
Mkurugenzi mkuu wa EWURA akizungumzia athari ya kuanza kushuka kwa thamani ya dola ya marekani kutokana na jitihada zinazofanywa na serikali kuinusu shilingi ya Tanzania, Je jitihada hizi zinaathiri vipi bei ya mafuta?